top of page

Swahili | Kiswahili

Updated: Sep 19, 2024

12 Things Parents Can Do to Prevent Addiction


Zana hii inaelezea mikakati ya uzuiaji kwa njia rahisi ambayo wazazi na walezi wanaweza kujumuisha katika maisha ya kila siku, ili kufanya tuwezalo kuwalinda watoto wetu dhidi ya uraibu baadaye maishani.


Addiction and the Brain


Uraibu ni hali ya kiafya inayoathiri ubongo na kubadilisha tabia ya mtu. Neno la kimatibabu la uraibu wa dawa za kulevya au pombe ni tatizo la matumizi ya vileo.


How Addiction Hijacks the Brain


Kuna sehemu kuu mbili za ubongo zinazoathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya: mfumo wa ubongo unaochochea hisia na koteksi. Mfumo wa ubongo unaochochea hisia, ulio kilindini mwa ubongo, huhusika katika silika zetu za kimsingi za kustahimili. Koteksi ni kitengo cha maamuzi na udhibiti wa msukumo.


How to Practice Refusal Skills


Fanya mazoezi ya utumaji ujumbe muhimu ambao vijana wanaweza kutumia katika hali hatari. Kwa mfano, mazungumzo kuhusu jinsi ya kukabili msukumo kutoka kwa wanarika wenzao au watu wengine kunywa au kutumia dawa za kulevya kwa kutoa majibu mahususi yanaweza kusaidia kuwatayarisha vijana kukabiliana na hali hizo. Kuna aina tano tofauti za ujuzi wa kukataa. Fanyia mazoezi ya chaguo zinazokufaa zaidi. Kijana wako aliyebaleghe anaweza kuigiza au kuandika majibu ambayo yanafaa zaidi.


Teens and Opioids


Matumizi ya opiodi huathiri sehemu muhimu ya ubongo ambayo hudhibiti ufanyaji wa maamuzi, kujidhibiti na mchakato wa kujipa raha.



 

Ukweli Kuhusu Fentanyl: Kuelewa Hatari

Facts About Fentanyl: Understanding the Risks





Fentanyl inapoendelea kuathiri jamii kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kuelewa uwezo na hatari zake ni muhimu ili kupunguza madhara. Kwa kuongeza uhamasishaji na kukuza hatua za kuokoa maisha kama naloxone, tunaweza kujitahidi kuzuia matumizi ya kupita kiasi na kuokoa maisha.



Kifafanuzi hiki cha video kinaangazia ongezeko la kutisha la opioidi sanisi kama vile fentanyl, hatari za overdose, ongezeko la tembe ghushi zilizo na fentanyl nchini kote, na umuhimu wa ufikiaji wa naloxone na elimu ya kuzuia overdose.

bottom of page